Kocha
wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Sebastien Migne amekitaja kikosi
cha wachezaji 30 ili kuanza maandalizi ya michuano ya kuwania ubingwa
wa mataifa ya Afrika, michuano itakayofanyika nchini Misri kuanzia
mwezi Juni.
Kikosi
hicho kinatarajiwa kwenda nchini Ufaransa kuanza maandalizi ya
michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Migne
raia wa Ufaransa, amemwacha nje beki David ‘Cheche’ Ochieng na
mshambuliaji wa Zesco United nchini Zambia, Jesse Were.
Christopher
Mbamba, anayechezea klabu ya Oskarshamns AIK nchini Sweden, ameitwa
kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Harambee Stars.
Mshambuliaji
Allan Wanga, ana kibarua cha kumridhisha kocha Migne kuwa katika
kikosi cha mwisho cha wachezaji 23, pamoja na Michael Olunga, Masoud
Juma na Ayub Timbe.
Harambee
Stars ambayo imepangwa katika kundi moja na Algeria, Senegal na
Tanzania, itakwenda kuanza maandalizi jijini Paris na kuondoka tarehe
18 kwenda nchini Misri, siku tano kabla ya michuano hiyo.
Kikosi
cha awali:-
Makipa:
Patrick
Matasi (St. Georges, Ethiopia), Faruok Shikhalo (Bandari FC, Kenya),
John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya), Brian Bwire (Kariobangi
Sharks).
Mabeki:
Philemon Otieno (Gor Mahia-Kenya), Musa Mohammed (Nkana FC-Zambia),
Joash Onyango (Gor Mahia-Kenya), Abud Omar (Sepsi Sfântu-Romania),
David Owino (Zesco United-Zambia), Bernard Ochieng (Vihiga
United-Kenya), Brian Mandela (Maritzburg United-Afrika Kusini), Erick
Ouma (Vasalund IF-Sweden).
Viungo
wa Kati: Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs-England), Anthony
Akumu (Zesco United-Zambia), Eric Johanna (IF Bromma-Sweden), Ismael
Gonzales (UD Las Palmas-Spain), Francis Kahata (Gor Mahia-Kenya),
Dennis Odhiambo (Sofapaka FC-Kenya), Johanna Omollo (Cercle
Brugge-Belgium), Christopher Mbamba (Oskarshamns AIK-Sweden),
Whyvonne Isuza (AFC Leopards, Kenya), Clifton Miheso (Ureno).
Washambuliaji:
Paul Were (AFC Leopards-Kenya), Ayub Timbe (Beijing Renhe-China),
Michael Olunga (Kashiwa Reysol-Japan), Allan Wanga (Kakamega
Homeboyz-Kenya), John Avire (Sofapaka), Masud Juma (Libya), Ochieng
Ovella (IF Vasalund, Sweden).